Mabingwa watetezi Real Madrid wanakutana na wapinzani wao wa mji mmoja Atlectico Madrid kwenye nusu fainali ya Champions League.
Real wataanzia nyumbani Mei 2 na kisha kurudiana ugenini Mei 10 ambapo mechi hizo mbili zitakuwa ni vita ya aidha kuendeleza ubabe au kukata uteja.
Real Madrid iliifunga Atletico mwaka 2014 na 2016 kwenye fainali na pia ikawatupa nje katika hatua ya robo fainali mwaka 2015.
Juventus ya Italia itakutana na Monaco ya Ufaransa katika nusu fainali nyingine.Baada ya kupangwa hatua ya nusu fainali, ilifuata hatua ya kusaka ni mshindi wa nusu fainali ipi atapewa hadhi ya kucheza kama mwenyeji kwenye fainali itakayochezwa Cardif Juni 3. Bahati ikawaangukia Juventus na Monaco.