Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

MO MUSIC AWATAKA MASHABIKI KUKAA MKAO WA KULA... amficha aliyempa shavu kwenye wimbo wake ujao

$
0
0
MKALI wa bongofleva, Mo Music amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kusubiri ujio wake mpya katika kibao ambacho amefanya na msanii aliyeamua kuficha jina lake hadi hapo kibao hicho kitakapotoka.

Akiongea na saluti5, Mo Music amesema kwamba kuna kazi kali inakuja ambayo amefanya kwa kumshirikisha mmoja wa wasanii wakubwa, lakini hata hivyo analiweka kapuni jina la msanii huyo hadi kibao hicho kitakapoachiwa rasmi.


“Kama Mo Music nawaomba mashabiki na wapenzi wangu wote wakae mkao wa kula kwani kazi mpya iko jikoni na wakati wowote itaiva na kupakuliwa,” amesema msanii huyo anayetamba na kazi zake nyingi zenye ubora wa hali ya juu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles