KOCHA wa timu ya taifa Ufaransa, Didier Deschamps ameafiki kuwa kiungo wake, Paul Pogba alichemsha kwenye mechi ya ushindi ya Bulgaria mwishoni mwa wiki iliyopita na kumtaka kuboresha kiwango chake.
Les Blues walipata ushindi wa kwanza kwenye mechi hiyo ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018, shukrani kwa mabao mawili kutoka kwa Kevin Gameiro, Dimitri Payet na Antoine Griezmann.
Pogba alikuwa muhimili katika nafasi ya kiungo kwenye michuano kwenye Euro 2016 lakini juzi alichemsha.
“Anaweza kufanya vizuri zaidi na lazima abadilike,” alisema Deschampis.
“Anapokuwa na majukumu ya kuingo mkabaji na akacheza vile, hicho siyo kiwango chake.
“Ana kila sababu ya kufanya vizuri anasifa ambazo wengine hawana.”