KIUNGO wa Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan amesema kwamba anataka kukipiga katika klabu ya Manchester United.
Kwa mujibu wa wakala wa nyota huyo, Mino Raiola nyota huyo wa timu ya taifa ya Armenia, atapatikana kwa bei poa kutokana na kwamba mkataba wake na vinara hao wa Ligi ya Bundesliga unatarajiwa kumalizika majira ya joto yajayo na huku Raiola akithibitisha kwamba nyota huyo hana mpango wa kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, Dortmund wameshasema kwamba hawana mpango wa kumuuza staa huyo mwenye umri wa miaka 27 wakati wa usajili wa majira haya ya joto, lakini wakala wake anasema kwamba suala la kujiungana Jose Mourinho kwenye klabu hiyo ya Old Trafford, bado linawezekana.