Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

LEICESTER CITY WAJIPA MATUMAINI YA JAMIE VARDY KUBAKI

$
0
0
MAKAMU wa rais wa Leicester City, Alyawatt Srivaddhanaprabha,amesema ana imani kwamba staa wao, Jamie Vardy atakataa kwenda kujiunga na Arsenal na badala yake ataendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu England msimu uliopita.

Msimu uliopita Vardy alizifumania nyavu mara 24 na kuwafanya mbwa mwitu hao kutwaa ubingwa huo wa Ligi Kuu bila kutarajiwa na jitihada zake zikamfanya aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England inayoshiriki michuano ya fainali za Mataifa ya Ulaya “Euro 2016”.

Mbali na hilo, pia kiwango alichokionyesha akiwa na Leicester City ndicho kilichoivutia Arsenal ambayo inasema kuwa tayari kulipa fedha za kuvunja mkataba na staa huyo kwa kiasi ambacho kinasemekna kuwa ni pauni mil 20 na huku ikisubiriwa Vardy atoe uamuzi wake wa mwisho baada ya kumalizika fainali hizo zinazofanyika nchini Ufaransa.

Hata hivyo, makamu huyo, Srivaddhanaprabha ambaye ni mtoto wa mmiliki wa klabu hiyo, Vichai, anaamini Vardy ataendelea kubaki na klabu hiyo ya King Power wakati Leicester City ikijiandaa kuwa moja ya klabu kubwa Ulaya.

“Utapata taarifa hivi karibuni lakini nadhani atabaki,” kibopa huyo aliliambia gazeti la The Daily Mail.


“Nadhani itakuwa hivyo, ngoja tuone. Tunahitaji kujenga timu. Bado tunaamini tunaweza kufanya kitu cha ajabu katika michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya,” aliongeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>