Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

ZINEDINE ZIDANE AMWANIA TENA EDEN HAZARD

$
0
0
EDEN Hazard amekiri kutaka kuendelea kubaki kuitumikia Chelsea msimu ujao, lakini kocha wa sasa wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepanga kumng’oa ili aweze kutua Santiago Bernabeu.

 Hazard mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akipambana kwa ajili ya kuifanya Chelsea irejee katika ubora wake pia kujihakikishia kubaki Stanford Bridge, lakini Zidane ameonyesha kuwa hafanyi mzaha kwa ajili ya straika huyo.

Imebainika kuwa Zidane amemweka katika rada za usajili wa kiangazi na ameweka dau la pauni 24 mil mezani kwa ajilki ya kufanikisha dili hilo.

Kwa mujibu wa Daily Telegraph, Hazard alikuwa katika mpango wa kuondoka katika usajili wa mwezi Januari, laini alikata shauri ya kubaki darajani hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Ninachoweza kusema ni kwamba, ni lazima Hazard atue Madrid, hii ni bada ya kuwakosa nyotakadhaa niliokuwa nikiwawinda.”

“Ni miongoni mwa wachezaji ambao sisi kama klabu lazima nikiri ndio ninaowawinda kwa ajili ya usajili wa majira ya joto,” amekiri Zidane.

Lakini kwa upande wake, bosi wa The Blue, Guus Hiddink alimzungumzia Hazard kama ni mshambuliaji asiyekata tamaa kulingana na aina ya mchezo, hivyo ni muhimu kuwa nae kikosini.

“Ni sawa na kusema Eden Hazard amerejea katika kiwango chake halisi, ni kati ya wachezaji ninaopenda kuwa nao kikosini, anatambua majukumu yake.”


“Anashika maelekezo kwa umakini na anawaongoza wenzake katika wakati ambao timu inahitaji matokeo. Tunapambana kwa ajili ya kuendelea kuwa nae hapa,” alisisitiza Hiddink.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>