Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

BREAKING NEWS!! VAN GAAL ATIMULIWA MANCHESTER UNITED

$
0
0
Louis van Gaal has been sacked by Manchester United just two days after leading the club to the FA Cup
Manchester United imemtimua kazi kocha wake Louis van Gaal siku mbili tu baada ya kutwaa taji la FA Cup Jumamosi iliyopita kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace.

Van Gaal ametimuliwa kufuatia mwenendo wake mbovu kwenye Premier League na nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho.

Benchi lake la ufundi la Waholanzi wenzake Albert Stuivenberg na kocha wa makipa Frans Hoek nao pia wamefungashiwa virago.

Ed Woodward aliwasili kwenye ngome ya mazoezi ya Manchester United - Carrington training complex kwaajili ya maongezi na Van Gaal Jumatatu asubuhi kabla ya muda mfupi baadae kutangaza kuwa kocha huyo ametimuliwa. 

Mourinho anatarajiwa kuwa na maongezi ya mwisho na Manchester United Jumanne kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitatu huku wasaidizi wake  Rui Faria na kocha wa makipa  Silvino Louro nao wakitarajiwa kumfuata Old Trafford.

Hatma ya kocha msaidizi Ryan Giggs bado iko inaelea hewani ingawa kuna kuna habari zinazodai kuwa Mourinho bado angependelea kuwa naye.
Louis van Gaal has been sacked by Manchester United just two days after leading the club to the FA Cup
Louis van Gaal amefukuzwa kazi Manchester United 
Van Gaal was pictured arriving at United's Aon Training Complex on Monday morning ahead of his sacking
Van Gaal akiwasili kwenye uwanja wa mazoezi muda mfupi kabla hajatimuliwa

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>