SHAMSA Ford alisema kuwa kuvaa nguo fupi sio kipimo kwamba ana tabia mbaya bali ni jambo la kawaida na kila mtu ana mtindo wa mavazi anaoupenda.
Mwigizaji huyo wa filamu alisema kuwa kuna baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimsema vibaya kwamba hafai kwa sababu anavaa nguo fupi.
“Kuna watu wanajifanya kuwa wananijua sana, kitu abacho si cha kweli na kumbe asilimia kubwa wamenijulia kwenye filamu, hivyo wakosoe kazi zangu na sio mavazi,” alisema Shamsa.
Aliongeza kuwa uamuzi wa kuvaa anavyojisikia ni wake mwenyewe ilimradi anazingatia utu na maadili kwa vile uamuzi wa kuvaa uko chini yake na kwamba watu wamkosoe katika kazi zake kama zina mapungufu na sio mavazi.