ZUWENA Mohammed ‘Shilole’ amesema kuwa haoni aibu kuzungumza lugha ya Kiingereza kwa makosa akidai kuwa anafanya hivyo kama njia mojawapo ya kujifunza kutokana na makosa.
Alisema, Kiingereza sio lugha mama ya Mtanzania hivyo haoni taabu kuongea ‘broken English’ na kwamba anajitahidi kufahamu kadri anavyoweza.
Video za Shilole akizungumza Kiingereza cha kuchapia zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii na kuwa burudani kwa watu wengine.
“Si mnaonaga wenyewe muda mwingine nisipoongea Kiswanglish changu watu wanaanza kunitafuta… ooh Shishi tafadhali ongea bhana, tunataka uongee,” alisema shilole alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha radio.