Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

JURGEN KLOPP AMFUKUZIA SERGIO RAMOS

$
0
0
MAJOGOO wa Jiji la London, wanapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia nyota wa Real Madrid, Sergio Ramos, laini wanalazimika kuweka dau la ziada mezani la pauni 24 milioni kwa ajili ya jembe hilo.

Ramos amekuwa akihusishwana kujiunga na Liverpool katika usajili ujao wa dirisha la Januari, lakini Liverpool inabidi kupambna kwa ajili ya kiungo huyo ambaye pia anawaniwa kwa karibu na Manchester United.

United wanatajwa katika dili la kumfukuzia nyota huyo wa Real Madrid kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha Mashetani Wekundu hao.

Lakini tarifa zinasema kuwa tayari kocha Jurgen Klopp ameshamaliza mazungumzo ya awali ya kiungo huyo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kinachopambana kwa ajili ya kuirejesha klabu katika hadhi yake ya miaka ya awali.

Awali, Liverpool waliweka mezani dau la pauni 15 mil. Kwa ajili ya Sergio Ramos kabla ya Madrid hawajaweka bayana kuwa dau la kiungo huyo ni 45 mil.

Bado Liverpool wanakomaa na dau la awali lakini wakaweka bayana kuwa wanaweza wakaongeza kiasi cha pauni 2 milioni ili dili kufikia pauni 12 milioni.

Ramos amekuwa katika kiwango bora katika kipindi cha miaka miwili hii na kuwa na uhakika wa kuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>