Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

AISHA VUVUZELA: NIMEISUBIRI KWA MUDA MREFU NAFASI YA KUITUMIKIA JAHAZI

$
0
0

Mwimbaji mpya wa Jahazi Modern Taarab, Aisha Vuvuzela amesema aliisubiri kwa muda mrefu nafasi ya kuitumikia bendi hiyo.

Vuvuzela aliyasema hayo Jumamosi iliyopita wakati alipofanya mahojiano na kipindi cha taarab cha luninga ya TBC1 chini ya mtangazaji Mariam Migomba.

“Nilisubiri kwa muda mrefu nafasi ya kujiunga na Jahazi, nadhani ni wasanii wengi wanaotamani kujiunga na Jahazi,” alisema Vuvuzela.

“Maombi yangu ya kujiunga na Jahazi yapo pale tangu nilipoondoka Mashauzi Classic, lakini nafasi yangu ilikuwa bado haijawadia.”


“Haikuwa rahisi kwangu kukataa kujiunga na Jahazi pale nafasi hiyo ilipowadia,” aliongeza Vuvuzela wakati akifafanua sababu za yeye kuondoka Wakali Wao Modern Taradance.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>