Manchester United imechelewesha shangwe za ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa Leicester City baada ya sare ya 1-1 ndani ya Old Trafford baina ya timu hizo mbili.
United ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 8 kupitia Anthony Martial lakini Leicester City ikazawazisha dakika 11 baadae mfungaji akiwa ni nahodha Wes Morgan.
Kama Leicester City ingeshinda mchezo huo, basi moja kwa moja wangekuwa ni mabingwa wapya wa England, lakini kwa sare hiyo sasa klabu hiyo imebakiza pointi mbili tu kutoka kwenye michezo yao mitatu iliyobakia ili kutwaa ubingwa.
Kimahesabu klabu pekee inayoweza kufikia pointi 77 za Leicester City ni Tottenham yenye pointi 69 ambayo ili iwe bingwa, inapswa kushinda michezo yake yote na Leicester City ipoteze mechi zote.
Tottenham inacheza na Chelsea Jumatatu usiku na iwapo matokeo yatakuwa sare, basi Leicester City itajikuta ikichukua ubingwa nje ya uwanja.
Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Lingard (Mata 61mins), Rooney, Fellaini (Herrera 74), Martial, Rashford (Depay 82)
Leicester: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez (King 88), Kante, Drinkwater, Schlupp (Albrighton 77), Okazaki (Gray 66), Ulloa

Leicesteri imeshindwa kutwaa taji kwenye uwanja wa Old Trafford

Wes Morgan akishangilia bao lake la kusawazsisha

Wafungaji wa mchezo huo Anthony Martial (katikati) na Morgan (kulia) wakipeana pongezi baada ya mchezo

Martial akiifungia United

Martial anakimbia kushangilia goli lake

Martial aliipa wakati mgumu Leicester wakati Manchester United ipotangulia kufunga