
LOUIS VAN GAAL amesema kwamba Leicester City kutwaa ubingwa ni jambo zuri kwa Premier League, lakini akaapa kikosi chake cha Manchester United hakitokubali kufanywa ngazi na timu hiyo kwa kuwa wapo vitani kuwania kumaliza msimu katika “Top Four”.
Kocha huyo Mholanzi anataka kuahirisha ‘pati’ ya Leicester City, wakati itakapokwenda Old Trafford Jumapili, ikijua kwamba ushindi utawahakikishia kuwa mabingwa wa Premier League kwa mara ya kwanza katika historia yao.
"Nadhani ni jambo zuri kwa Premier League na soka kwa ujumla, kwamba si mara zote timu hizo hizo zinakuwa mabingwa… Nilikuwa wa kwanza kusema kwamba wanaweza kuwa mabingwa, hivyo kwangu si ajabu.
"Lakini hatuwezi kuruhusu watangazie ubingwa Old Trafford. Nadhani kwamba watakuwa mabingwa wiki ijayo,hivyo sisi hatutaki “kuvuruga” pati yao, ni kuiahirisha kidogo tu," alisema.