RIYAMA Ally amesema kuwa tangu ajitose kwenye Bongo Muvie mwaka 2000, siku ya kwanza ya kuona matunda ya sanaa ilikuwa ni baada ya kuigiza vema kama mtoto aliyegeuzwa kichaa na mama yake mzazi.
Riyama alisema kuwa nafasi hiyo alicheza katika Tamthilia ya ‘Jabali’, iliyokuwa ikionyeshwa na runinga ya ITV, ambayo ilikuwa ikimzungumzia mama aliyechanganya dawa alizopewa na mganga ili ampe baba yake.
“Matokeo yake dawa hizo nikapewa mimi na hivyo kujikuta nikiwa kichaa… kwakweli kila nikikumbuka Tamthilia hiyo huwa najisikia rah asana kwasababu ndio iliyonitambulisha kwani niliitendea haki,” alisema Riyama.
Alisema kuwa pamoja na umaarufu alionao sasa kwenye filamu, ni lazima akumbuke alikotoka kwamba amepitia mabonde na milima hadi kufikia kuwa na jina kubwa.