STAA wa Bongo Movie, Yobnes Yusuph ‘Batuli’, amewataka wanaume wenye nia ya kweli ya kuoa wasiwaogope wasanii na badala yake wajaribu bahati yao.
Amesema katika utafiti wake amebaini kuwa wanaume wengi wanahofia kuwaoa watu wenye majina makubwa kwa kuamini kwamba wakiwaoa watakuwa wameumia kwa vile baadhi ya wasanii nyota wamekuwa wakionyesha mifano mibaya kwenye jamii.
“Lakini napenda kuwatoa wasiwasi kwamba sio wote wana tabia mbaya, ni baadhi tu na mtu akitaka kuoa ni lazima achunguze, hivyo waoaji nao wafanye hivyo badala ya kuogopa tu,” alisema Batuli.
Alisema, wapo wasanii wengi wa kike wenye tabia njema kuliko wenye tabia zisizo njema, hivyo ni suala la kuwachunguza tu.