Onyesho la pamoja la mahasimu wakubwa wa muziki wa dansi Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” na Msondo Ngoma Music Band “Baba ya Muziki” litakalofanyika Jumamosi hii, limeibua majigambo na mabishano makubwa kutoka kambi za bendi hizo.
Msondo na Sikinde wataumana kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe (sasa hivi CDS Park) kuanzia saa 11 jioni na kuendelea hadi usiku mnene.
Onyesho la safari hii limenoga zaidi baada ya bendi hizo zote mbili kupata ‘air time’ ya kutosha kupitia kipindi kipya cha muziki wa dansi Afro TZ kinachorushwa na Radio One Stereo kila siku za Jumatatu hadi Alhamisi saa 4 usiku mpaka saa 7 usiku.
Kupitia kipindi hicho, Sikinde na Msondo ziliweza kunadi vizuri silaha zao pamoja na majigambo ya kila namna.
Wakati Mjusi Shemboza wa Sikinde akiiambia Saluti5 kuwa kuiangusha Msondo ni lazima, Ridhawan Pangamawe wa Msondo nae ameiambia Saluti5 kwamba Sikinde kwao ni kama kumsukuma mlevi.
Yote kwa kwa yote, haijawahi kutokea ‘mechi’ ya Sikinde na Msondo kudoda, huwa ni nyomi la kufa mtu na burudani iliyokwenda shule. Mbona kitanuka TCC Club Jumamosi hii!
Zifuatazo ni picha 28 za onyesho la mahasimu hao lililofanyika mwaka jana Julai 18 TCC Club. Hebu jikumbushe uhondo ulivyokuwa
Zifuatazo ni picha 28 za onyesho la mahasimu hao lililofanyika mwaka jana Julai 18 TCC Club. Hebu jikumbushe uhondo ulivyokuwa
Hassan Rehan Bitchuka wa Sikinde akiwa jukwaani
Shaaban Dede wa Msondo akifanya yake
Hassan Moshi TX jr akiwajibikwa kwenye jukwaa la Msondo Ngoma
Bitchuka
Mwimbaji Abdallah Hemba wa Sikinde akiwa na tabasamu pana
Ali Jamwaka akizigonga tumba za Sikinde
Wadau wa muziki wa dansi William Kaijage (kushoto) na Said Mdoe wakifuatilia kwa makini mpambano wa Msondo na Sikinde. Aliyepakatwa ni Sahad Mdoe
Athuman Kambi mmoja wa waimbaji tegemeo wa Msondo
Juma Katundu wa Msondo akiimba moja ya nyimbo zilizotingisha kwa sana
Kutoka kushoto: waimbaji wa Sikinde Hassan Kunyata, Munsemba na Abdallah Hemba
Shaaban Lendi wa Sikinde akitesa na Saxophone lake
Abdallah Hemba wa Sikinde akipozi na mchezaji wa zamani wa Yanga Mohamed Hussein Mmachinga
Kushoto ni shabiki maarufu wa Yanga Ali Yanga akijipoza na machungu ya kufungwa na Gor Mahia kwenye Kagame Cup
Shabiki akipagawa na solo la Kaingilila Maufi wa Sikinde
Kutoka kushoto ni Mbaraka Othman, Juma Mbizo na Hassan Kunyata
Mjusi Shemboza akifurahi na gitaa lake la kati
Mjusi Shemboza wa Sikinde akiendelea na makamuzi
Mnyupe mpulizaji pekee wa ala za upepo kwenye jukwaa la Msondo katika onyesho hilo
Mashabiki wakiendelea kuburudika na ngoma za Sikinde na Msondo
Tony mpiga bass wa Sikinde
Mwimbaji wa Msondo Juma Katundu (kushoto) akiwa na seneta wa Msondo Abdulfareed Hussein Tazama umati wa watu uliofurika TCC Club
Waimbaji wa Msondo kutoka kushoto ni Kambi, Dede, Hassan Moshi na Juma Katundu
Hawa ndio makamanda wa Saluti5 waliochukua matukio yote ya onyesho la Msondo na Sikinde Jamal Said Mdoe (kushoto) na Abdallah Mensah
Rajab Zomboko kutoka Radio One ndiye aliyekuwa MC wa wa onyesho hilo
Rajab Zomboko kutoka Radio One ndiye aliyekuwa MC wa wa onyesho hilo