Manchester United inapiga hatua za haraka ili kuhakikisha kiungo wa Benfica Renato Sanches anatua Old Trafford msimu ujao na kuzipiku Real Madrid na Paris Saint-Germain ambazo nazo zinawania saini ya kinda huyo.
Swali sasa ni je Renato Sanchez ana uwezo wa kuichezea timu kama Manchester United? Mchambuzi Goncalo Lopes wa Daily Mail la Uingereza anasema jibu ni "NDIYO".
Goncalo Lopes anasema: "Naamini hakuna 'kipaji' kingine kilichozaliwa Ureno baada ya Cristiano Ronaldo zaidi ya Sanchez. Renato Sanchez ndiyo mbadala wa Ronaldo".

Manchester United inakaribia kumnsa kinda wa Benfica na Ureno Renato Sanches (kulia)

Sanches amekuwa kwenye msimu mzuri Ureno tangu alipopandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Benfica