Mwimbaji, mtunzi na mwanamuziki mwandamizi wa Mashujaa Band, Jado FFU ametangaza kuachana na bendi hiyo aliyoshiriki kuiasisi zaidi ya miaka mine iliyopita.
Jado ametangaza hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook masaa kadhaa yaliyopita huku akisema kuwa mwanamuziki mmoja aliyemkaribisha kundini ndiyo chanzo cha yeye kuamua kuachana na Mashujaa.