Ama kwa hakika Akudo Impact bado ni Vijana wa Masauti, wimbo wao mpya kabisa “Wanawake” utakudhihirishia kuwa bendi hii bado iko vizuri.
“Wanawake” ni kazi iliyosukwa kwa ushirikiano wa wanamuziki wote na kisha ikarekodiwa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitshou Bampadi ambaye pia ndiye mkung’utaji gitaa la salo wa Akudo.
Pata wasaa wa kuusikiliza wimbo huo “Wanawake” kutoka kwa Akudo Impact “Vijana wa Masauti”.