Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

RAHEEM STERLING ASEMA AMEFUATA MATAJI MANCHESTER CITY

$
0
0
RAHEEM STERLING amesema ameachana na Liverpool na kujiunga na Manchster City kwaajili ya kushinda mataji.
City imemtambulisha rasmi winga huyo wa England baada ya kukamilsha usajili wake wa pauni milioni 49 ambao unamfanya awe mchezaji ghali zaidi kutoka England. 
MATAJI: Sterling anasema amekwenda Manchester City kushinda mataji
Sterling ataingiza kitita kizito cha pauni 180,000 kwa wiki katika mkataba wake wa miaka mitano, lakini nyota huyo anasema hicho sicho kilichompeleka City bali amefuata mataji.
Sterling, 20, anasema: "Ni furaha ilioje kutua City? Wachezaji wenye kiwango cha kidunia wako hapa na kikosi kinakidhi vigezo vya kushinda mataji mwaka hadi mwaka.
"Wachezaji bora kabisa wanakuzunguka, kuna kila kitu unachokihitaji hapa cha kukupeleka kwenye 'level' nyingine, hivyo hakuna cha kujutia."
HUKU NDO KWENYEWE: Sterling rasmi ndani ya Etihad 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles