
Tajiri mkubwa zaidi barani Afrika, Aliko Dangote ameushtua ulimwenngu baada ya kutangaza nia ya kuinunua Arsenal ya England.
Dangote anaweza kuwa hajulikani sana na mashabiki Waingereza lakini ana pesa za kutosha kutimiza ndoto yake iwapo mwanahisa mkubwa wa Arsenal Stan Kroenke ataamua kuuza hisa zake.
NI NANI HASA ALIKO DANGOTE?
Ana umri wa miaka 57 mzaliwa wa Nigeria anamiliki makampuni makubwa ya sementi, unga na sukari. Dangote anategemewa kwenye sukari Nigeria kwa asilimia 90 katika nchi hiyo yenye wakazi milioni 170 - hayo ni mauzo makubwa kupindukia.
Dangote pia anajenga kiwanda kikubwa cha kusafishia mafuta ambacho kitakamilika mwaka 2018
DANGOTE ANA UTAJIRI WA KIASI GANI?
Jarida la Forbes limemweka kama mtu wa 67 kwa utajiri duniani akiwa na hazina ya pauni bilioni 12. Utajiri wake ni mara mbili ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ambaye anashika nafasi ya 137.
Alizaliwa kwenye familia ya wafanyabiashara katika jiji la Kano ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Nigeria. Akiwa na umri wa miaka 21, mjomba wake akampa mkopo wa kuanzisha biashara yake mwenyewe.
NI MTU MUHIMU KIASI GANI?
Forbes inamtaja kama mtu mweusi wa pili mwenye nguvu duniani baada ya rais wa Marekani Barack Obama.
STAILI YA MAISHA YAKE IKOJE?
Anaishi kwenye jumba lake la kifahari lenye madirisha ya kuzuia risasi huko kwenye kisiwa cha Victoria, sehemu ya kitajiri zaidi Nigeria katika jiji la Lagos. Ni Muislam, amesomea biashara katika Chuo Kikuu cha Cairo, Misri na ana watoto watatu huku akiwa mpenzi mkubwa wa kufuga 'mustachi'.

Dangote anatajwa kama tajiri mkubwa kuliko wote Afrika

Dangote katika picha ya pamoja na binti yake Halima huko New York mwaka jana

Lango la kuingilia kwenye kiwanda cha cement cha Dangote kilomita 50 kutoka jijini Dakar, Senegal

Dangote anaingiza pesa nyingi kutoka kwenye viwanda vyake vya cement, sukari, unga pamoja na mafuta huko Nigeria

Habari hii imetafsiriwa na Saluti5, ukiamua kuichukua tupe heshima yetu tafadhali kwa kututaja kama chanzo.